RAMLA MASALI, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara katika Mkoa wa Mtwara kuanzia tarehe 14 mpaka 17 mwezi septemba 2023.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini Kwake leo septemba 9,2023 .
“ Mh Rais pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo anatarajia kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini pia kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.”
“Lakini pia kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi yalitotolewa kwa yakati tofauti”. amesema Kanali Abbas
Kanali Abbas amewaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi kumlaki Dkt Samia Suluhu Hassan Katika maeneo yote atakayopita lakini pia wajitokeze kwa wingi katika mikutano.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






