BRYSON MSHANA, MTWARA

www.mtwarapressblog.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali  Amamed Abbas, amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani utakaotumika kwenye ununuzi wa zao la Mbaazi msimu 2023/2024 unalenga kumnufaisha mkulima kupata soko la uhakika.

Kanali Abbas amesema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa mazao ya mbaazi mkoa wa mtwara, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Boma Mtwara Julai 31, 2023.

Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, wakulima watakusanya Mbaazi na kuuza kwa pamoja kupitia vyama vyao vya ushirika kwa ajili ya kupata bei nzuri inayoendana na soko.

“Mfumo huu ni sehemu ya juhudi za serikali kumtafutia soko mkulima, hivyo ukasimammiwe vizuri ili kuhakikisha kuwa makato yawe ni yale tu yaliyopitishwa kisheria hivyo utasaidia kuyaelekeza katika shughuli za maendeleo ya wananchi zilizopitishwa” ameeleza Kanali Abbas.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kwa wajili ya kufungua kikao, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanafi Msabaha, amesema ni jambo jema kuona Mkoa unategemea zao zaidi ya moja la uchumi hali inayochangia kuendelea kukuza kipato cha wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Hali hii imechangia kuongeza muamko wa wanachi katika kulima mazao mengine zaidi ikiwepo Mbaazi na Ufuta, tofauti na awali ambapo zao moja tu la Korosho ndio lilikuwa linapewa kipaombele” amesema DC Msabaha

Kwa mujibu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi Mtwara (MAMCU) kimesema kimejiandaa vizuri na Msimu wa Mbaazi 2023/2024 na tayari imeshaagiza vifungashio ambavyo vinatarajiwa kuwasili ifikapo Tarehe 05/08/203.

Taarifa ya MAMCU iliyowasilishw akwenye kikao na Kaimu Meneja wa MAMCU Tawi la Masasi Costantine Francis, imeeleza kuwa imewekwa makisio ya kununua Mbaazi Tani 15,000 kutoka vyama 187 ambavyo vitashiriki katika ununuzi wa zao hilo kwa msimu huu.

Kwa upande wa baadhi ya Wakulima walioshiriki kikao hicho wameonesha kuridhishwa na mfumo huo wakieleza kuwa unafaa kuungwa mkono na changamoto zitakazojitokeza zitaendelelea kutatuliwa kulingana na muda unavyoenda.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Bi. Hawa Mkata Mkulima kutoka Kijiji cha Chigugu Wilayani Masasi, ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye zao la Mbaazi, akieleza kuwa utakuwa na manufa kwa wakulima wote ikiwepo wale wa wadogo.

“Kwa kuanzia kunaweza kuwa na changamoto ambazo zitaendelea klutatuliwa polepole, hata wakati tunaingiza Korosho kwenye mfumo ilikuwa hivyohivyo lakini wote sasa tunaona mafanikio ya mfumo huu, nashauri tuingie kwa aslimia 100 mfumo huu ni mkombozi wa mkulima” Amesisitiza Hawa Mkata

 

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…