RAMLA MASALI, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Taifa Steven Wasira, amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya mambo makubwa kwa muda mchache, ikiwa ni pamoja na kujenga Madarasa bure bila kuchangisha wazazi.

Amezungumza hayo julai 16, 2023, uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, kupitia Mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo, Kanda ya Kusini.

Wasira amesema Mambo makubwa yanayofanywa na Dkt. Samia ni Pamoja na kujenga Madarasa bure, kujenga Barabara pamoja na Mradi wa kujenga bwawa la Mwalimu Nyerere Rufiji ambao ujenzi wake umefikia asilimia 90.

“Wakati Hayati Magufuli anafariki aliacha ujenzi huo ukiwa asilimia 30 na sasa ni 90 utakamilika hivi karibuni.“ Amesema Wasira.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…