RAMLA MASALI, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Gavana Annis Chamsidine kutoka kisiwa cha Anjouan kilichopo Nchini Comoro akiambatana na Madiwani wa eneo hilo, wamewasili Mkoani mtwara kwa ziara ya kibiashara.

Pamoja na mambo mengine ziara hiyo pia inalenga kudumisha mawasiliano mazuri Katika visiwa vya Comoro na Tanzania, hasa katika nyanja za biashara, huduma za usafiri pamoja Elimu.

Wakati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, Gavana huyo ameelezea baadhi ya changamoto wanazokumbana na Raia wa Comoro wanapokuja Tanzania, kuwa ni pamoja na usumbufu wa masuala ya Viza na kutakiwa kulipa pesa ili waachwe katika maeneo wanayofanyia biashara.

“ingekuwa nzuri mazingira yakawekwa sawa ili wafanya biashara wafanye biashara vizuri bila changamoto na wengine wenye Meli wanacheleweshwa kushushiwa mizigo yao Bandarini.”Amesema Annis

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, amesema Tanzania na Comoro zitaendeelea kushirikina katika mambo mbalimbali ikiwemo Biashara , Elimu na Kilimo kama njia ya kudumisha ushirikinao kwa Nchi hizo mbili.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…