HADIJA OMARY, LINDI
mtwarapreeclub@gmail.com
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, Sokoine, Dkt. Alexander Makalla, amesema kijana Simon Manyoli, aliyejikata Uume amehojiwa hospitalini hapo na kudai kuwa alifanya kitendo hicho kutekeleza maelekezo aliyopewa kutoka ‘juu’.
Amezungumza hayo Julai 12, 2023 alipokua akihojiwa na Wanahabari juu ya maendeleo ya mgonjwa huyo na kuongeza kuwa maelezo ya mgonjwa ni kwamba amekuwa akipewa maelekezo kutoka juu na kwakua yeye ni mfalme mwaminifu anatekeleza maagizo hayo.
Kuhusu hali ya Mgonjwa, amesema kutokana na tatizo lake la afya ya akili, licha ya kuanza kuongea na kutembea lakini bado wauguzi na wataalam wa magonjwa ya akili wanaendelea na matibabu kuhakisha afya yake inakaa sawa na kwamba hawawezi kumruhusu mgonjwa huyo kurudi nyumbani mapema kwa kuhofia kuendelea kujidhuru zaidi.
Amesema wakati huu amewekewa mpira kwaajili ya kumsaidia kupata haja ndogo na kupona majeraha yake vizuri asipate maambukizi kwenye kidonda, na baada ya wiki mbili mpira huo utatolewa na hivyo atakuwa yupo sawa.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






