BRYSON MSHANA, TABORA
Timu za mikoa ya Mwanza na Singida zimeingia fainali ya mchezo wa Soka maalum wasichana, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea Mkoani Tabora.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumapili Tarehe 11 Juni 2023 Saa 2 Asubuhi kwenye uwanja A wa Shule ya Sekondari Wavulana Tabora, Timu ya Mkoa wa Singida iliibuka na ushindi baada ya kuifunga Geita Goli 1- 0.
Mchezo mwingine ulichezwa kwenye uwanja C majira ya saa 2 Asubuhi na kuzikutanisha timu za mikoa ya Mwanza na Mara, ambapo Timu ya Mkoa wa Mwanza iliibuka mshindi kwa jumla ya magoli 4 – 0.
Kwa upande wa Soka Maalumu Wavulana, timu ya mkoa wa Kigoma imeingia fainali baada ya kuifunga Kagera magoli 3 -2, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja A Tarehe 11 Juni 2023 Saa 4 Asubuhi.
Mchezo wa kuhitimisha hatua ya nusu fainali Soka maalum Wavulana ulizikutanisha Dar es salaam na Shinyanga, na kumalizika kwa Dar es salaam kuingia fainali baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1.
Kwa matokeo hayo sasa, Timu za Mikoa za Soka maalum kutoka Mikoa ya Singida na Mwanza zitakutana katika Fainali, huku Soka maalum wavulana ikizikutanisha Kigoma na Dar es salaam.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






