BRYSON MSHANA, TABORA
Timu kutoka Mikoa mbalimbali zimeanza kushindana katika michezo ya UMITASHUMTA 2023 iliyoanza Juni 03, 2023 Mjini Tabora.
Michezo hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya shule za Sekondari Tabora wasichana na wavulana, inajumuisha mpira wa Netibali, Mpira wa Wavu (wasichana na Wavulana), Mpira wa miguu kawaida (Wasichana na wavulana), Mpira wa miguu wavulana (Maalum) na Mpira wa mikono – Handball (kawaida).
Vilevile inahusisha Mchezo wa kuruka chini, Riadha (kwaida na maalum) Mpira wa Goli (Goal Ball) mahususi kwa wenye uono hafifu, Mpira wa kikapu (Wasichana na Wavulana) na Sanaa za michezo zinazojumuisha uimbaji na uchezaji wa ngoma za asili.
Katika michezo iliyochezwa leo, uwanja A wa Shule ya Sekondari wavulana Tabora, timu ya mpira wa miguu Wasichana Mkoa wa Dodoma ilikutana Manyara na kutoshana nguvu kwa kutofungana.
Upande wa Mpira wa Kikapu wasichana, Timu kutoka mkoa wa Pemba imeibuka na ushindi wa vikapu 14 dhidi ya 7 vya Mkoa wa Shinyanga, katika mchezo wa kusisimua uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari wavulana Tabora.
Mchezo mwingine wa mpira wa miguu wasichana ulishuhudia Mkoa wa Simuyu ukiibuka na ushindi wa magoli 2, dhidi ya Morogoro iliyopta goli 1, huku Kilimanjaro ikiibuka na ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Katavi.
Kwa upande wa soka wanafunzi wenye mahitaji maalum, Timu ya Mkoa wa Kilimanjaro ilishinda Dar es Salaam kwa magoli 4 -1, na katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye uwanja C Shule ya Wavulana Tabora.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA mwaka 2023, yanaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






