MWANDISHI WETU, NACHINGWEA

www.mtwarapressblog.co.tz

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Liondi Adinani Mpyagila ametangaza kuchukuliwa hatua kwa  vikundi vyote ambavyo vimekuwa havirudishi mikopo ya asilimia 10 wanayokopeshwa na Halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya LAAC wilayani Nachingwea Machi 20, 2023, Mwenyekiti huyo amesema kumekuwa na vikundi vingi vinakopa lakini vinashindwa kurudisha fedha hizo kwa wakati au mara nyingine wasirudishe kabisa.

Mpyagila amesema Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea itaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vyote kama ambavyo serikali imeagiza, lakini watakuwa makini na wakali kwa wanavikundi wote wadanganyifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa amesema kuwa watakuwa makini wakati wa kutoa mikopo ya asilimia 10 ili kuepukana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata kutoka kwa wananchi waliokopa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mhandisi Kawawa amesema kuwa kamati ya LAAC imewapa nguvu na njia muhimu za kufuatilia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kila kikundi kinarejesha mkopo kwa wakati na vikundi vingine viendelee kukopa.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…