MWANDISHI WETU, MTWARA
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas amesema kuwa kilele cha Juma la elimu la elimu mkoa wa Mtwara kinatarajiwa kufanyika Machi 15 na 16 Mkoani Mtwara ambapo kitahimizishwa na Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda.
Akizungumza na waandhishi wa habari Mchi 14, 2023 ofosini kwake,Kanal Ahmed Abbas amesema kuwa hali ya mahudhurio ya wanafunzi shuleni ni nzuri na wamejitokeza kwa wingi shuleni.
“Mahudhurio ni mazuri na vijana wamejitokeza kwa kiasi kikubwa naona tumepiga hatua kwa kiwango kikubwa kwenye ufaulu ambapo sio jambo jepesi sana hii ni sehemu ya jitihada ambazo tumefanya na tumejiridhisha kuwa tuko vizuri”
“Kwakweli tumedhamilia kufanya mabadiliko makubwa kwa vijana wetu kwa muda mrefu kwenye utoaji wa elimu ya msingi na sekondari tumekuwa hatufanyi vizuri   ambapo mwaka 2021 tuliweka malengo saba ya kipaumbele ikiwemo kuendesha juma la elimu na kutoa tuzo kwa walimu na wanafunzi walionyavizuri zaidi ambappo ni maadhimisho ya pili kwa mwaka huu”
“Maadhimisho haya yameanza kwanza kufanyika kwa ngazi ya kata ambapo tarehe 15 tutafanya kilele kwa kuendesha makongamano, midahalo maonyesho ya kitaaluma michezo na sanaa ttc na tareh 16 itakuwa maadhimisho kimkoa ambapo atakuwa waziri wa elimu”
“Lengo likiwa ni kuhakamasisha na kuamsha hali ya ufundishaji na ujifunzaji ili kufikia malengo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni tuwajibike kwa pamoja kuleta maendeleo ya elimu”
Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Kiduma Mageni amesema kuwa walifanya utafiti ambapo na kubaini  baadhi ya vikwazo kwenye elimu.
“kwa sekondari mwaka 2021 asilimia 7.4 lakin 2022 asilimi 6.2  ambapo wazazi na wanafunzi wakishirikiana juma la elimu linachangia sana kuwaweka pamoja”
Katika ufaulu darasa la saba ufaulu umepanda kutoka 75.63 hadi 76.63 kwa msingi lakini kwa sekondari ilikuwa kidato cha nne waliofaulu ni asilimia 88.63 mwaka jana 93.20.
“Walifaulu kwa ubora wa hali ya juu 1-3 ilikuwa asilmia 29.0 mwaka jana 34.84  uwezo umeongezeka hili kwetu ni fanikio kubwa kidato cha sita hatuna 0”

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…