MWANDISHI WETU, NEWALA
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas amefurahishwa na juhudi za  Chama Kikuu cha Ushirika TANECU kujenga kiwanda cha ubanguaji wa korosho Wilayani Newala, ambacho kinatarajia kukamilika  mwezi April mwaka huu.
Akizungumza wakati  akitembelea kiwanda hicho Machi 10, 2023 Kanal Abbas amesema kinaenda kuwa mkombozi wa wakulima  wa zao hilo ambapo sasa wataweza kuuza korosho ghafi katika Chama hicho.
“Ndio maana tunasema fikirieni kuongeza thamani kwenye mnyororo mzima wa zao la korosho yaani tuna maanisha kila kitu kuanzia ubanguaji ambapo  tunaweza  kuwa na bidhaa tofauti tofauti  na kubangua pekee hii ndio maana ya Ushirika” alisema Kanal Abbas
Nae Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika TANECU Mohamed Nassoro amesema kuwa wanatarajia kujenga  Viwanda 10 ambavyo vina tarajia kubangua   Zaidi ya Tani 3500 Kwa mwaka ambapo  wanatajis watapata  korosho karanga Zaidi ya  Tani 856 Kwa mwaka.
“Tunalengo la kujenga Viwanda 10  kama hivi na vikikamilika vyote tunatarajia kubangua Tani 35,000 Kwa mwaka thamani ya jengo bil1.25 kuanzia mitambo inathamani ya shilingi  bilioni 1.800 ambapo tumepanga kikikamilika tuanze kubangua korosho chache hasa zile ambazo wananchi wanazo majumbani” amesema Nassoro
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu TANECU Bwana Karim Chipola, amesema kuwa kukamilika Kwa Viwanda hivyo kutaenda kusaidia wakulima.
“Yaani tunafanya kwa vitendo Ili kumsaidia mkulima wa zao la korosho kubangua korosho yake nchini na kulinufaisha Taifa  ndio maana  hata matumizi yetu mengi tumeyabana Ili tuweze kukamilisha mradi huu”.amesisitiza Chipola.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…