MWANDISHI WETU, MTWARA

www.mtwarapressblog.co.tz

Wakulima wa zao la Korosho kata ya Njengwa, Halmashauri ya Mji Nanyamba, wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kuanika Korosho zao kabla ya kuzipeleka sokoni ili kuongeza ubora.

Akizungumza Machi 10, 2023 katika mkutano wa kutoa elimu kwa wakulima wa kata hiyo juu ya masuala ya ushirika na kilimo kwa ujumla, mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Cooperatove Union (MAMCU), Siraji Mtenguka, amesema korosho nyingi za wilaya ya Mtwara zinakabiliwa na unyevu mkubwa kutokana na kuwa katika ukanda wa Pwani.

“Kwahiyo kimsingi inatakiwa huku kuongezeke nguvu ya kipekee ya jitihada kubwa katika kuanika Korosho zetu, kwahiyo nilikua najaribu kutoa elimu hapa na wakulima wananielewa kuhusu kuanika Korosho na kudarajisha korosho kuweka katika ‘standard’ inayokua inafaa na wanunuzi inayowavutia zaidi.” Amesema Siraji Mtenguka.

Nao baadhi ya wakulima akiwamo Esha Nammwena, amesema tatizo linalopelekea korosho kuwa na unyevu ni ukosefu wa elimu kwa baadhi yao na kushindwa kuelewa umuhimu wa kuanika korosho zao.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…