BRYSON MSHANA, MTWARA
Manispaa ya Mtwara – Mikindani mkoani mtwara, imetoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 27.21 kwa watu Saba wenye ulemavu wa aina mbalimbalimbali ili kuwawezesha katika kufanya shughuli za maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya, amekaeeleza kuwa mkopoa huo alioukabidhi desemba 09, 2022 ni sehemu ya asilimia 10 inayotolewa na serikali kupitia mapato ya halmashauri kwa wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.
DC Kyobya amesema mkopo huo umetolewa ikiwa ni katika kusherehekea miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika, huku akiwataka wanufaika kuendelea kushirikiana wao wenyewe kwa wenyewe na kuhakikisha kuwa wanafanya marejesho kwa wakati.
Kundi linguine lililokabidhiwa mikopo ni la wanawake, ambapo jumla ya vikundi 24 vya Wanawake vilipata mkopo wenye thamani ya shilingi Milioni 157.248 huku Vijana wakipata Milioni 60.411
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






