BRYSON MSHANA, MTWARA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Zawadi Ally Mohamed (24) mkazi wa Kijiji cha Nanyanga Wilaya ya Tandahimba kwa tuhuma za mauwaji ya Ally Mohamed Zawadi (59) ambaye ni baba yake mzazi, baada ya kutokea mgogoro wa fedha za ufuta.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara SACP ISSA J. SULEIMAN tarehe 29 Julai 2025, imesema kuwa mtuhumiwa alitekeleza kitendo hicho tarehe 26 Julai 2025 kwa kumchoma marehemu na kitu chanye ncha kali maeneo ya tumboni, shingoni na kwenye bega la kulia hali iliyompelekea majeraha na kusababisha kifo chake.

Katika hatu nyingine Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia Rashid Issa Mula (50) mkazi wa kijiji cha Mnazi Mmoja Wilaya ya Nanyumbu, kwa tuhuma za mauwaji ya Joseph Hassana (42), yaliyotokea tarehe 23 Juni 2025 baada ya mtuhumiwa kumvizia marehemu akiwa Nyumbani kwake na kumpiga kwa kutumia kitu butu kichwani na kusababisha majeraha yaliyopelekea kifo chake.

Chanzo cha mauwaji hayo ni baada ya mtuhumiwa kumtuhumu marehemu kumuibia mwiko wa kupikia, ambapo baada ya kutekeleza mauwaji hayo mtuhumiwa alikimbilia kijiji jirani cha Msumbiji ili asikamatwe.

Aidha kupitia Opareshine na misako, Jeshi la Polisi mkoani Mtwara  limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 14 wakiwa na kilogramu 16, msokoto mmoja na kete 145 za dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni bangi.

Katika msako huo pia wamekamatwa watuhumiwa wane wakiwa na jumla ya lita 250 za pombe haramu ya moshi (Gongo) pamoja na pikipiki mbili zenye usajili wa Mc 551 EWD aina ya Boxer na Mc 737 BVW aina ya Sanlg ambazo zilikuwa zikitumika kusafirisha pombe hizo.

taarifa hiyo ya Jeshi la Olisi iliyotolewa kwa vyombo vya habari pia imeelezea hukumu zilizotolewa na Mahakama katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara, ikiwemo ile ya tarehe 11 Julai 2025 ambapo mahamaka ya Wilaya ya Nanyumbu ilimhukumu kifungo cha miaka 60 jela Yasin Abdallah Lakini (25) mkazi wa kijiji cha namasongo Wilaya ya Nanyumbu baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kidato cha pili (jina la mwanafunzi na la shule limehifadhiwa).

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya Mhe. Asifiwe Crespo Jembe na mwendesha Mashtaka Deusdedith Ngobetse, ambapo  Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilomnamo mwezi machi 2025 katika Kijiji cha Namangasongo, kata ya Chipuputa baada ya kumlaghai mwanafunzi huyo kwa kumpatia zawadi ndogondogo kisha kumbaka.

Aidha Tarehe 10 Julai 2025, Mahakama ya Wilaya ya Masasi mkoani mtwara ilimhukumu kifungo cha miaka 20 jela Thomas Gabiriel Khamis (31) mkazi wa Kijiji cha chingulungulu baada ya kumtia hatiani kwakosa la kupatikana na Nyara za Serikali.

Mtiwahatiani huyo alikutwa na Nyara hizo za Serikali  tarehe 28 Januari 2025 nyumbani kwake kijiji cha Namatutwe akiwa na Ngozi saba za mnyama aina ya Ngolombwe na magamba 23 ya Kakakuona bila ya kuwa na Kibali. ambapo hukumu ya kesi hiyo ilitolewa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya Mhe.A.R Ndosy na mwenesha Mashtaka Karimu Mioraji.

Kupitia taarifa yake ya julai 29, 2025 kwa vyombo vya habari, Jeshi la Polisi mkoani mtwara limeendela kuwataka wananchi kutii sheria na kuacha kujichukulia sheria Mkononi, badala yake watumia niia sahihi za kutatua migogoro na kumaliza tofauti zao ikiwa ni pamoja na kushirikisha Taasisi zenye mamlaka kisheria.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…