Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawi la Mtwara Nassoro Omary akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Siku tatu inayoambatana na mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kutoka Zanzibar, Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Ruvuma inayofanyika kwenye ukumbi wa BOT Mtwara kuanzia Tarehe 25-27 Februari 2025.

BRYSON MSHANA, MTWARA

Benki Kuu ya Tanzania – BOT imesema itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika vyombo mbalimbali ya habari nchini, ili kuwajengea uwezo wa kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu  biashara, uchumi na fedha.

Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawi la Mtwara Nassoro Omary, ameeleza hayo tarehe 25 Februari 2025 wakati akifungua Semina ya Siku tatu inayoambatana na mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kutoka Zanzibar, Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Amesema kuwa BOT inatambua mchango wa wanahabari katika kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii kupitia uandishi wa habari, ndio maana wamekuwa wakiandaa utaratibu wa kukutana nao kila mwaka kwa ajili ya kukumbushana mambo muhimu yanayohusu uchumi na fedha.

“Ni matumaini ya Benki Kuu kuwa kukutana huku kutakuwa na manufaa makubwa, kwa waandishi wa habari wanaoshiriki watapata fursa ya kukutana na wataalm mbalimbali na kujifunza kwa ajili ya kwenda kuwaelimisha wananchi wengine” amesema Nassoro Omary.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa semina hiyo Ndg. Bryson Mshana ameishukuru BOT kwa kuendeleza utaratibu wa kukutana na waandishi wa  habari kila mwaka, kwa ajili ya kuwakumbusha masuala muhimu yanayohusu fedha, uchumi na biashara hali ambayo imewapa urahisi katika kuwaelimisha wananchi.

“Semina hizi zinazoambatana na mafunzo kutoka kwa wataalam wa Benki Kuu zimekuwa zikifanyika kwa miaka kadhaa sasa, na zimekuwa msaada mkubwa kwa wanahabari hawa na wengine sio katika kuandika tu lakini kuwa na mawasilaino ya moja kwa moja na watendaji wa benki kuu ambao  wamekuwa wakitoa msaada wa kihabari wakato wowote”

Naye Dominick Mwita Mchumi kutoka BOT aliyewasilisha mada za Muundo na Majukumu ya BOT pamoja na Sera ya fedha inayotumia Riba ya Benki Kuu, amesema mfumko wa bei nchini uko chini ya lengo la 5%, ambapo kwa January 2025 ilikuwa 3% sawa na ilivyokuwa Disemba 2024.

Noves Moses ambaye ni Meneja msaidizi Idara ya mawasilaino BOT, ameeleza umuhimu wa semina hiyo kwa waandishi wa habari na namna ambavyo imekuwa na faida kwa waandishi wa habari na wananchi kwa takribani miaka 17 tangu ianze kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…