BENKI KUU YA TANZANIA – BOT

Benki Kuu ya Tanzania imetoa tahadhari kwa taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila kuwa na leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sharia.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanznaia Disemba 31, 2024 imeeleza kuwa kifungu 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, ni kosa kwa taasisi, kampuni na watu binafsi kujihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila kuwa na leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Kifungu cha 16(2) (a) cha Sheria hiyo kimeainisha adhabu inayopaswa kutolewa kwa kuendesha biashara ya kukopesha bila kuwa na leseni ikiwa ni pamoja na kutozwa faini isiyopungua Shilingi milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili au vyote viwili kwa pamoja.

Benki kuu Imesisitiza juu ya Umma kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambaye hana leseni, na endapo taasisi au mtu binafsi anataka kufanya biashara ya ukopeshaji anatakiwa kufuata taratibu husika za kuomba leseni kutoka Benki Kuu ili apewe kwa mujibu wa Sheria.

Orodha ya taasisi zenye leseni za kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu pamoja na leseni

za mikopo ya kidijiitali zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu, kupitia ukurasa wa:

https://www.bot.go.tz/Other/Orodha%20ya%20Watoa%20Huduma%20Ndogo%20za%2

0Fedha%20wa%20Daraja%20la%20Pili.pdf.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…