MWANDISHI WETU, RUANGWA
mtwarapressclub@gmail.com
Chama kikuu cha ushirika RUNALI kinacho hudumia wilaya za Nachingwe, Ruangwa na Liwale Mkoani Lindi, kimekabidhi jumla ya madawati 143 klwa Halamshauri ya Wilaya ya Ruangwa ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kurejesha faida wanayoipata kwa jamii.
Madawati hayo yamekabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma leo Tarehe 10 February 2024, ambaye ameeleza kuwa hali hiyo inaendelea kuonesha kwa vitendo juhudi za kuunga mkono serikali katika kukuza elimu wilayani humo.
DC Ngoma ametumia nafasi hiyo kuishukuru RUNALI Kwa mchango huo wa madawati, ambao amesema kuwa utawafikia na kuwasaidia zaidi ya wanafunzi 4 wanaosoma katika shule mbalimbali Wilayani Ruangwa.
“Tunawashukuru sana wadau wetu hawa wa elimu kwa hiki walichokifanya, mchango huu utasaidia sana kukuza elimu sambamba na watoto kukaa kwa idadi inayotakiwa hali itakayochangia ukuaji wa elimu katika Wilaya yetu”
“Hiki mlichokifanya kinaifanya jamii kuona umuhimu wa ushirika, hakuna mkulima ambaye anaweza kusema hauoni umuhimu wa ushirika wakati mambo mazuri kama haya yanafanywa na chama chao, hili ni jambo jema na narudia tena kuwapongeza RUNALI” amesisitiza DC Ngoma
Kwa upande wake mwenyekiti wa Runali Bw. Odas Mpunga, ameeleza kuwa wanachokifanya ni kutimiza moja ya misingi yao ya kurudisha huduma kwa jamii, akieleza kuwa chama hicho kinayo misingi saba kilichojiwekea katika kuhudumia jamii katika maeneo kinchoyahudumia.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa RUNALI ilitenga bajeti ya shillingi million 30 kwa ajili ya kuchangia huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa Ruangwa, Nchingwea na Liwale akizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na uchangiaji wa madawatina vifaa vya ujenzi katika shule mbalimbali.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






