MWANDISHI WETU, NANYAMBA
mtwarapressclub@gmail.com
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara, wameeleza kutoridhishwa kwao na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa madai ya kupuuza hoja zinazo wasilishwa kwenye vikao vya baraza la madiwani.
Madai ya madiwani hayo yameibuka kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kujadili utendaji kazi wa kata cha robo ya pili ya mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Februari 9, 2024.
Diwani wa kata ya Nitekela Salumu Issa Chihediwe,amehoji taarifa ya kamati ya fedha kuhusu kiasi cha fedha kilicho kopwa kutoka kwenye kiwanda cha tofali kinachomilikiwa na Halmashauri hiyo kutofafanua matumizi yake na jumla ya kiasi kilicho kopwa.
Chihidiwe pia memuomba Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji Nanyamba kupitia baraza hilo kukaa kwa pamoja na kumjadili Mkurugenzi huyo ambae anakwenda kinyume na utaratibu wa utumishi.
“Sikubaliani na maagizo haya ya kamati ya fedha,kwasababu maagizo yalipuuzwa ya kikao kilichopita na kikao hiki tunaagiza tena,naomba kupitia baraza lako la madiwani kwa niaba ya wajumbe wenzangu huyu mtumishi hadi kikao cha kamati ya fedha hao watu wawe wameshalipwa hiyo fedha.”
“Kwasababu ni mzoefu ametajwa Mkurugenzi na mkaidi wa kushindwa kutekeleza maagizo ya kamati na mabaraza nina ushahidi wa hivyo vitu,mwenyekiti baraza lako kwakua huyu ni mtumishi kama watumishi wengine tugeuke tujadili taarifa zake kwa kina kuhusu mtumishi huyu kwanini anakwenda kinyume na utaratibu wa utumishi.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la madiwani Jamali Kapende amesema kupitia kikao cha kamati kilichojadili utendaji kazi wa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambapo maadhimio ya kikao hicho madiwani wameomba wenye mamlaka yenye dhamana ya mkurugenzi watafute namna ya kumpeleka maeneo mengine.
“Hayo ndio maazimio yaliyofikiwa na madiwani kutika kujigeuza kutoka baraza kuwa kamati hayo ndio maadhimio yao,wenye mamlaka husika wataona kwenye muhtasari iliyoandikwa.”Amesema Kapende
Kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mtwara vijijini Didas Zimbihile,amewaomba watunza kumbukumbu za vikao kutengeneza muhtasari wa kikao husika.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






