RYSON MSHANA, MASASI
mtwarapressclub@gmail,com
Kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Mtwara, kimefanyika katika Wilaya ya Masasi Desema 10, 2023, kikihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya anyumbu Dkt. Stephan Isaac Mwakajumilo, aliyemuwakilisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas.
Kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili mkoani Mtwara, imeandaliwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mtwara chini ya Mtandao wa MTWANGONET kwa kushirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mtwara.
Katika hotuba yake Dkt. Mwakajumilo ameeleza kuwa kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Mkoa wa Mtwara, imefanyika kwa ushirikiano wa Serikali na Wadau wote zikiwemo Asasi za Kiraia na kufanya shughuli mbalimbali za kupinga vitendo vya ukatili.
Amesema jumla ya watoto 6,906 wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19, wamepata ujauzito mkoani Mtwara ndani ya miezi 10, kuanzia Januari hadi Oktoba 2023.
“Kwa mujibu wa takwimu za mfumo wa taarifa wa upashanaji wa habari za afya (MTUHA) katika Mkoa wa Mtwara kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba 2023 watoto 6,906 wenye umri kati ya miaka 10 na 19 walipapata ujauzito.” Amesema Dkt. Mwakajumilo
Aidha, Mwakajumilo amesema Vitendo vya ukatili wa kinjisia Mkoa wa Mtwara vimezidi kuongezeka kwa mwezi Januari mpaka Septemba 2023 ambapo jumla ya matukio 1,120 yameripotiwa dawati la jinsia.
Kati ya matukio hayo, ya watu wazima yaliyoripotiwa ni 436, wanawake 536, wanaume 100 na watoto 684.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Door of Hope Clemence Mwombeki amesema kwa sasa wameweka mipango madhubuti ya dhana shirikishali kwa jamii ili kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa makundi yote kutoka kwenye Jamii.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






