HADIJA OMARY, LINDI
Ini ni kiungo muhimu ndani ya mwili wa binadamu, kikiwa na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya 500 mwilini, mojawapo ikiwa ni kuchuja na kuondoa sumu kwenye Damu.
Ini linaweza kupata shida na kuvimba na kusababisha homa ya Ini (Heptitis) kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo Matumizi ya Pombe kupita kiasi.
Wataalamu wanaeleza kuwa moja ya njia za usambaaji wa Homa hiyo ya Ini ni kutoka kwa Mama Kwenda kwa motto, ambapo inaelezwa kuwa Mama aliye na Maambukizi ya Hepatitis B humuambukiza Mtoto baada ya kujifungua.
Kusipokuwa na juhudi za matibabu za mapema za kuzuia maambukizi ya homa ya ini, kuna uwezekano wa hadi asilimia 90 kwa mama kumuambukiza Mtoto.
Mratibu wa Afya ya uzazi na Mtoto Kutoka kituo cha Afya cha Mji kilichopo Manispaa ya Lindi Mkoani humo Bi Farida Ibrahimu, anawashauri akina Mama kuwahi cliniki pindi wanapojihisi kuwa ni wajawazito ili waweze kupata chanjo ikiwemo ya homa ya Ini pamoja na ushahuri wa afya ya uzazi ili kuepukana na changamoto za maradhi kwa watoto watakao jifungua.
Mratibu huyo alisema kwa mama kuwahi kliniki pindi tu anapojihisi kuwa ni mjamzito, kulingana na vipimo vya awali atakavyofanyiwa ataweza kujua kama ana maambukizi ya aina yoyote ambayo yanaweza kumuathiri mtoto alie tumboni au la na hivyo kuweza kumlinda mtoto huyo kitaalam mpaka atakapo zaliwa.
“katika maeneo hatari zaidi duniani virusi vya hepatitis b (hbv) kwa kawaida usambazwa kupitia kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususani nyakati za utotoni “iwapo hamna juhudi za kitiba za kuzuia maambukizi kuna uwezekano hadi asilimia 90 kwa mama alie na maambukizi ya hepatitis b kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua”.
Anasema kama ilivyo kwa virusi vya ukimwi virusi vya homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate,jasho na mwingiliano wa damu ya mtu mwenye virusi hivyo hivyo endapo mama mjamzito hatapata chanjo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ni rahisi kwa Mtoto atakae jifungua kupata maambukizi hayo.
Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine http://sokoinerrh.go.tz/ imielezea homa ya ini kuwa ni janga linaloua kimya kimya ambapo kulingana na takwimu za vifo duniani inakadiriwa kirusi cha Ini aina ya B pekee huua watu 600,000 kila mwaka.
kwa wastani watu Zaidi ya bilioni mbili, sawa na asilimia 33 ya watu wote ulimwenguni, wameambukizwa Virusi vya HBV, na wengi wao hupona baada ya miezi michache, huku watu milioni 350 wakiendelea kuwa na virusi hivyo wengi wao wakiwa hawaoneshi dalili na kuendelea kuambukiza watu wengine .
Katika maeneo ya Bara la Afrika Tanzania ikiwemo maambukizi ya virusi vya homa ya Ini ndio sababu kuu ya shida kwenye Ini.
Virusi vya homa ya Ini vipo vya aina 5 (A,B,C,D, na E) ingawa aina mbili za Virusi hivyo ( B na C ) ndio sababu kuu ya Ugonjwa wa Homa ya Ini kusambaa kupitia Damu na Maji maji ya mwili.
Kuwahi kituo cha kutolea huduma za Afya mapema kwa mama mjamzito hasa yule mwenye maambukizi ya ugonjwa huu wa Ini pindi tu anaposikia hali ya uchungu ni mhuhimu ili wataalamu kuweza kufanya maandalizi ya awali kwa ajili ya kumkinga Mtoto atakaezaliwa kama anavyoeleza Grecy Mrope muuguzi mkunga katika kituo hiko cha Afya cha Mji
Mrope anaeleza kuwa Mama mjamzito anaweza kumkinga Mtoto wake asipate ugonjwa huo pale wahudumu au wataalamu wanapompatia huduma kipindi cha kujifungua kwa njia ya kawaida au ya upasuaji.
Anaongeza kuwa mtoto akishazaliwa anatakiwa kupewa dozi ya heptitis b imanune globenn hbig ndani ya masaa 12 ili kumkinga na homa ya ini.
“dozi hiyo inatakiwa apewe mara tatu, ambapo dozi ya kwanza atapatiwa ndani ya masaa 12 tangu azaliwe, dozi ya pili baada ya miezi sita na dozi ya mwisho ni baada ya mwaka mmoja kupita tokea mtoto huyo azaliwe” ameeleza
Virusi vya ugonjwa wa homa yaini vinaelezwa kuwa vinasambaa na kuambukiza Mtu mara 100 zaidi ya virusi vya UKIMWI, kama ilivyoelezwa katika tovuti ya Hospitali ya Mkoa wa Lindi Sokoine http://sokoinerrh.go.tz/, jambo linaloashiria kuwa bado ipo haja ya elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi.
Shuwea Juma mkazi wa manispaa ya Lindi anasema kuwa pamoja na ugonjwa huo wa ini kuwa ni ugonjwa hatari lakini bado elimu ya kutosha kuhusiana na ugonjwa huo haijafika kwa wananchi ambapo anasema uwenda maambukizi yakaendelea kuenea kwa kukosa Elimu.
“ mimi nadhani Elimu izidi kutolewa zaidi kwa wananchi juu ya ugonjwa huu kupitia kwenye vyombo vya habari hata mbao za matangazo na hata mashuleni kama ilivyo kwa magonjwa mengine kama vile ukimwi na hata corona ili wananchi tuchukuwe taadhari zaidi za ugonjwa huo. Alieleza Shuwea
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






