RAMLA MASALI, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas ameeleza kuwa uwekezaji wa Bandari uliofanywa na serikali ya awamu ya sita, umeongeza uwezo na ufanisi katika kuhudumia wateja mbalimbali waaotumia Banari ya Mtwara.
Kanali Ahmed Abas amesema hayo Mjini Mtwara Leo Jumamosi Septema 09, 2023 wakati akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA)
Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023 Bandari hiyo ililenga kuhudumia jumla ya tani za shehena ya mizigo 400, 002 , lakini lengo limevuka kwa asilimia zaidi 304 .92 kwa kuhudumia jumla ya tani 1, 628, 000.
Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni kuongezeka wateja wapya walioanza na walionesha nia ya kutumia bandari ya Mtwara, ikiwa ni pamoja na kampuni mbalimbali za kusafirisha mizigo zikiwepo za madini ya makaa ya mawe, malighafi za saruji, grafaiti pamoja na mazao kama Korosho, Mbaazi na Ufuta.
“ Sio hayo lakini pia TPA mmeongeza uwezo wa kuhudumia meli za kupakia tani elf 65, ukilinganisha na gati la mwanzo ambalo lilikua linapikia tani elfu 45 hili sio jambo dogo “amesema Kanali Abbas.
Katika hatua nyingine Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imekabidhi vifaa Tiba vikiwamo Vitanda vya kujifungulia (Delivery Beds) 15 kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Septemba 09, 2023 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Juma Kijavara, ikiwa ni muendelezo wa wiki ya mamlaka ya Bandari.
“Thamani ya vitu tunavyokwenda kuvitoa hapa ni Milioni 30 msaada ambao kwa ujumla utatolewa wa vifaa hivyo. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tunakuahidi sisi kama wana TPA tutaendelea kuunga mkono juhudi zako kama ambavyo wewe unatuunga mkono kwenye shughuli zetu za kila siku kwenye hilo tutakuwa bega kwa bega.” Amesema Mhandisi Kijavara.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dk. Lobikieki Kisambu, ameushukuru uongozi wa TPA kwa msaada huo ambao unakwenda kuboresha huduma za Mama na Mtoto.
“Wodi ya wazazi ya sasa iliyopo kwa wale ambao mmeshafika pale mnaona jinsi ambavyo iko finyu ina uwezo wa vitanda 35 tu, na tutakapoenda kupanua ile wodi basi itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda zaidi ya 130, kitu ambacho kitasaidia kuboersha huduma katika sehemu ya Mama na Mtoto.” Ameeleza Dk. Kisambu, akizungumzia uboreshaji wa majengo unaofanyika katika hospitali hiyo kongwe inayokwenda kutimiza miaka 59 mwezi ujao.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






