MOHAMED MWAYA, MASASI

mtwarapressclub@gmail.com

Chama kikuu cha ushirika wa Wilaya za Masasi, Mtwara na Nanyumbu (MAMCU LTD) kimefanya mnada  wa kwanza wa zao la mbaazikatika kijiji cha Mkululu wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Mnada huo Tarehe 11 Agusti 2023, ikiwa ni mara ya kwanza zao hilo la Mbaazi kuuzwa kupitia mfumo rasmi wa stakabadhi ghalani huku bei ya juu kwa kilo moja ikifikia shilingi 2,003 na bei ya chini 1,950.

Meneja Mkuu wa MAMCU LTD Biadia Matipa, ameelezea bei hiyo kuwa zuri na kuufanya kuwa mwanzo mzuri wa msimu wa Mbaazi 2023/2024.

“Kwa mara ya kwanza MAMCU LIMITED tumefanya mnada wa mbaazi na tunashukuru wakulima wameipokea vizuri bei ya mbaazi tunatoa wito Kwa wakulima kuepuka kuuza mbaazi kuptia utaratibu usio rasmi, ili kuepuka kudhulumiwa bei”Amesema Matipa.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa katika mnada huo wameipongeza serikali kwa kuendelea kuimarisha mifumo ya unuzi wa zao la Mbaazi, huku wakitoa wito wa utaratibu ulioazishwa kuedelea kusimamiwa ili uzidi kuleta tija kwa wakulima.

Bi Halima Bakari ni mmoja wa wakulima ambao wameuza Mbaazi kwenye mnada huo wa kwanza, ambaye ameeleza kuwa ameridhishwa na utaratiu uliotumika kwa sababu hauna tofauti na uuzaji wa mazao mengine kama Korosho na Ufuta.

“Huu sio utaratibu mpya, tumeutumia hata kweye mazao yetu megie na tumeshuhudia manufaa ya kuuza kwa stakabadhi ghalani, Serikali imefanya vizuri kuingiza na Mbaazi huko, mkulima ukiwa na kiasi chochote unapeleka kwenye chama chako” ameseam Halima

MAMCU imeweka makisio ya kununua Mbaazi Tani 15,000 kutoka vyama 187 ambavyo vitashiriki katika ununuzi wa zao hilo kwa msimu 2023/2024.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…