MWANDISHI WETU, KILIMANJARO

www.mtwarapressblog.co.tz

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amesema Serikali inatekeleza jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kutatua changamoto walizonazo.

Dkt. Kijaji amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Magodoro cha TANFOAM kilichopo Jijini Arusha kujionea shughuli za uzalishaji magodoro na kisikiliza changamoto walizonazo.

Aidha, Amesema Wizara yake inatekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambapo moja msingi yake ni kuondoa majukumu yanayofanana kati ya Taasisi ili kurahisisha ufanyaji biashara na uwekezaji nchini

Akiongea na uongozi wa kiwanda hicho, Dkt. Kijaji amezitaka Taasisi kuacha kufanya majukumu yanayofanana na kuzitaka kushirikiana katika kuwahudumia wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza biashara na uchumi wa Taifa

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa TANFOAM Bw Mechack Jimmy ameishukuru Serikali kwa jitahada mbalimbali inazozifanya katika kutatua changamoto za Wafanyabiashara na wawekezaji ili kuwawekea mazingira bora ya ufanyaji biashara na uwekezaji.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…