MWANDISHI WETU, KILIMANJARO
www.mtwarapressblog.co.tz
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) awataka Maafisa Biashara wote nchini kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria.
Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo.
Dkt. Kijaji amesema ni jukumu la Maafisa Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua.
Dkt. Kijaji amesisitiza kiwa ni jukumu la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya Juhudi za kila namna ili kuweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na mazingira bora na wezeshi ili kukuza biashara zao na kiwa na tija.
Aidha, amesema bidhaa zinazotengenezwa nchinj zinatakiwa kuwanufaisha wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na biashara yoyotee inayofanyika nje ya nchi inatakiwa kuwa rasmi.
Vilevile amekipongeza Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC kwa kutoa ajira zaidi ya elfu 3200 na jinsi kinavojihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii inayokizunguka
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha TPC, David Shiltu amesihi watanzania kuwa na Amani kwa kuwa sukari ipo sokoni ya kutosha na hakuna uhaba na uzalishaji unaendelea.
Akiwa Mkoani Kilimanjaro, Dkt. Kijaji amekitaka Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kuongeza uzalishaji wa bidhaa ili ziweze kukudhi mahitaji ya soko la ndani na soko la nje.
Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kitatua changamoto zilipo kiwandani hapo.
Aidha, Dkt Kijaji amesema bidhaa hizo kama Viatu, mabegi na mapochi zinazotengenezwa na Kiwanda hicho kwa kitumia malighafi za ndani ya nchi zina asilimia 100 ya kukishi vigezo vya kuingia katika soko la eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA).
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






