MWANDISHI WETU, ARUSHA

www.mtwarapressblog.co.tz

Waziri wa Viwanda Na Bishara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali inahakikisha sekta binafsi inaendelea kukua na hakuna kiwanda chochote kitakachofungwa ili kuendelea kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Taifa

Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 1, 2023, wakati  alipotembelea Kiwanda cha A to Z kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo na kusikiliza na kitatua changamoto walizonazo.

Aidha, Amewataka wafanyabiashara kuwa na ushirikiano na Serikali katika kutoa changamoto wanazozipata na watoe mapendekezo ya suluhisho za changamoto hizo kwa kuwa Serikali ipo tayari kuzishughulikia.

Akiwa Jijini Arusha pia Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vishikwambi cha Tanztech kwa lengo la kujionea uzalishaji huo na kusikiliza changamoto zao.

Akizungumza kiwandani hapo, amesema ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia TEHAMA katika mitaala ya elimu

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho cha Tanztech Bw. Gurveer Hans amesema Kiwanda hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali katika kutoa bidhaa hiyo mashuleni na kwa watu binafsi kwa bei nafuu.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…