MWANDISHI WETU, MBEYA
www.mtwarapressblog.co.tz
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amewasili Jijini Mbeya kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya Kilimo – Nane Nane 2023 yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Tarehe 01.08.2023 katika viwanja vya John Mwakangale.
Ufunguzi huo wa kitaifa unatarajiwa kuongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Mkuu huyo wa Wilaya ambeambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias, na kufanya ukaguzi wa mwisho wa Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Kwa Mujibu wa DC Mwanziva, kupitia maonesho hayo Wilaya yake imejipanga kuonesha bidhaa za Kilimo kwa mifano ya mazao mbalimbali yanayozalishwa Ludewa (Shamba Darasa na Bidhaa zake), kupitia Bustani ya kisasa ya mbogamboga.
Vile vile ameeleza kuwa wameandaa Bwawa la Samaki la Kisasa lenye aina mbalimbali ya Samaki wanaofugwa kupitia programu za Ufugaji wa Samaki Wilayani Ludewa, ambapo yupo mfugaji wa Mfano ambaye wameambatana naye kwa ajili ya maonesho.
Amewaomba wananchi kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewala ambapo pamoja na kujionesha shughuli mbalimbali za kilimo, lakini pia watapa kujua fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana wilayani humo.
Maonyesho hayo kwa mwaka 2023 yameambatana na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”. na yanfanyika katika kanda mbalimbali nchini, huku kitaifa yakifanyika Jijini Mbeya.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






