BRYSON MSHANA, TABORA
Mikoa ya Tabora na Dodoma, imefanikiwa kuingia fainali ya mpira wa miguu wasichana katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023).
Michezo ya Nusu fainali imechezwa Leo Tarehe 23 Juni 2023, ikizikutanisha Manyara na wenyeji Tabora ikimalizika kwa wenyeji Tabora kusonga mbele baada ya ushindi wa jumla ya magoli 3-1.
Katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa saa 4 Asubuhi, Dodoma na Mbeya zilimaliza muda wa kawaida zikiwa hazijafungana, hivyo kulazimika kutumika sheria ya mikwaju ya penati iliyoipelekea Dodoma kushinda kwa penati 5-4.
Kwa matokeo hayo, sasa fainali ya UMISSETA 2023 upande Soka Wasichana utazikutanisha Tabora na Dodoma, Mchezo utakaochezwa Tarehe 24 Juni 2023 kwenye uwanja mpya wa Shule ya sekondari Wavulana Tabora, majira ya Saa 3:20 Asubuhi.
Fainali hiyo itatanguliwa na mchezo wa kumtafuta atakayeshika nafasi ya tatu kati ya Manyara na Mbeya, utakaochezwa kwenye uwanja huohuo majira ya Saa 1:30 Asubuhi.
Erick Mfugale, Mkufunzi kutoka chuo Cha Michezo malya – Mwanza ambaye ni Mratibu wa mchezo wa Soka katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023), amesema kuwa maandalizi ya mchezo wa fainali yameshakamili na kinachosubiriwa ni muda tu ili kumpata Bingwa.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






