BRYSON MSHANA, TABORA
Mpira ya meza ni moja ya michezo inayochezwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) Mkoani Tabora, ambao vijana kutoka mikoa mbalimbali yameendelea kushindana.
Katika Michezo iliyochezwa Asubuhi ya Tarehe 19 Juni 2023 kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tabora Wasichana, Mkoa wa Kilimanjaro Wasichana ulishinda Manyara Wasichana kwa Seti 3-0 na Dar es salaam ikaifunga Pemba 3-0.
Mchezo Mwingine ulizikutanisha Unguja na Ruvuma Wavulana na kumalizika kwa Ruvuma kukubali kipigo cha Seti 3-0, kabla ya Wenyeji Tabora Wasichana kuifunga Mtwara Wasichana 3-0.
Michezo mingine miwili ya Wavulana iliwakutanisha Njombe na Mtwara, na kupelekea Njombe kuibuka na ushindi wa 3-0 kisha Dar es salaam ikawafunga Manyara 3-0.
Jumla ya Mikoa 16 inashiriki mchezo wa Meza katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023), hali inayoonesha kuendelea kukua kwa mchezo huu mashuleni.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






