BRYSON MSHANA, TABORA
Wawakilishi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wameanza kushindana katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) iliyofunguliwa Juni 15, 2023 Mjini Tabora.
Mashindano ya UMISSETA 2023, yanaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Michezo hiyo ilijumuisha mpira wa Netibali, Mpira wa Wavu (wasichana na Wavulana), Mpira wa miguu kawaida (Wasichana na wavulana), Mpira wa miguu wavulana (Maalum) na Mpira wa mikono – Handball (kawaida).
Vilevile ilihusisha Mchezo wa kuruka chini, Riadha (kwaida na maalum) Mpira wa Goli (Goal Ball) mahususi kwa wenye uono hafifu, Mpira wa kikapu (Wasichana na Wavulana) na Sanaa za michezo zinazojumuisha uimbaji, uchezaji wa ngoma za asili na Muziki wa Kizazi Kipya (Bongo Flavour).
Michezo iliyochezwa Tarehe 16 Juni 2023 ni pamoja na riadha ambayo katika hatua za awali mikoa imechauana vikali katika Mita 100 na Mita 3,000 Wasichana na Wavulana huku mikoa ya Arusha na Manyara ikionesha upinzani mkali.
Kwenye Netiboli Iringa iliifunga Singida magoli 39 – 20, Songwe ikaifunga Tabora 30 – 26, Geita 39 Kagera 11, Mwanza ikaifunga Mbyea 45 – 13, Simiyu ikashinda 34 – 27 dhidi ya Morogoro na Tanga ikaifunga Arusha 33 – 22.
Kwa upande wa mpira wa Wavu Mkoa wa Tabora ulishinda Seti 3 – 1 dhidi ya Arusha, Mbeya ikaishida Rukwa kwa Seti 3-0, Simiyu ikafungwa 3 – 0 na Dar es salaam, Lindi wakaibuka Kidedea dhidi ya Songwe kwa 3 – 0, Shinyanga ikaifunga Ruvuma 3 – 1 na Pwani ikaondoka na ushindi wa 3 – 0 dhidi ya Njombe.
Katika mchezo pendwa wa Soka Wavulana, Kagera na Mwanza zilitoshana nguvu kwa sare ya 2-2, Songwe ikakubali kipigo cha 2-0 kutoka kwa Tanga, Manyara ikaifunga Ruvuma 3-2, Pwani ikapokea kipigo cha 5 – 1 kutoka kwa Shinyanga na wenyekji Tabora wakaibuka na ushindi wa 2 – 0 mbele ya Kilimanjaro.
Mpira wa Kikapu Wavulana nao ulishuhudia michezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Pwani kuifunga Morogoro kwa vikapu 52-24, Mbeya ikaishinda Simiyu 29-25, na Arusha ikaishinda Kilimanjaro 30-23.
Michezo mingine ya Kikapu Wavulana Katavi iliifunga Mara 23-14, Mwanza ikaidhibu Shinyanga 76-15, Tabora ikaishinda Mtwara 19-17, Songwe wakakubali kipigo cha 34-6 kutoka Manyara na Pemba ikaishinda Ruvuma 46-18.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






