BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Timu za mpira wa miguu za wasichana kutoka mikoa ya Mwanza na Singida zimeendelea kufanya vizuri kwenye mshindano ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea Mkoani Tabora.

Katika mchezo namba 27 wa kundi A uliochezwa Tarehe 09 Juni 2023 kwenye kiwanja A Shule ya Sekondari Tabora Wavulana, Timu ya Mkoa wa Mwanza iliibuka na Ushindi mnono wa magoli 11-0 dhidi ya Mkoa Wa Ruvuma.

Mchezo mwingine ulikuwa wa kundi C ulioikutanisha Mikoa ya Singida na Iringa kwenye kiwanja C Shule ya Sekondari Tabora wavulana, na kushuhudiwa Singida ikiiadhibu Iringa kwa jumla ya magoli 8-0.

Kwa upande wa mpira wa Miguu Wavulana Timu ya Mkoa wa Mwanza iliibuka na ushindi wa magoli 3 – 1, baada ya kuifunga Timu ya Mkoa wa Mbeya kwenye mchezo wa kusisimua, huku Pemba ikiwafunga wenyeji Tabora 3-0.

Matokeo mengine Unguja ilipoteza 1-0 kwa Dar es salaam, Mtwara na Pwani zikatoshana nguvu kwa sare ya 1-1, na Kilimanjaro ikiwafunga majirani zao Arusha kwa 2-1 kisha Tanga ikaisambaratisha Katavi kwa 2-1.

Michezo ya UMITASHUMTA iliyoanza Tarehe 03 Juni 2023, inaendelea katika viwaja mbalimbali vilyopo shule za Sekondari Wavulana na Wasichaa Tabora, ikiwa inaingia katika hatua za fainali, nusu fainali na fainali.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…