BRYSON MSHANA, TABORA
Timu ya wasichana ya Mkoa wa Geita, imeibuka na ushindi mnono baada ya kupata ushindi wa magoli 8-0 dhidi ya Mkoa wa Songwe.
Mchezo huo wa kusismua umechezwa Asubuhi ya Juni 5, 2023 kwenye Uwanja B wa Shule ya Sekondari Wavulana Tabora.
Mchezo mwingine katika Uwanja A ulizikutanisha timu za mikoa ya Mwanza na Katavi, ukipelelea Mwanza kupata ushindi wa magoli 5-0, huku Singida ikipoteza 2-0 dhidi ya Mkoa wa Rukwa.
Kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma uliibuka na ushindi wa magoli 3-1, baada ya kuwafunga Iringa katika mchezo uliochezwa uwanja A wa shule ya Sekondari Wavulana Tabora.
Matokeo mengine Kilimanjaro iliwafunga majirani zao Arusha 3-0, Shinyaga ikakubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Simiyu, Manyara wakaifunga Morogoro 3-0, Kagera wakakubali yaishe bada ya kufungwa 3-1 na Mkoa wa Mara.
Wenyeji Tabora waliendelea kujiweka vizuri katika hatua ya Mkundi, baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mkoa wa Pwani kwenye mchezo wa kundi D, huku Tanga ikiifunga Mtwara 2-0.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






