BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Timu za mpira wa mikono wavulana na Wasichana za Mkoa wa Tabora, zimeendelea kufanya vizuri baada ya kupata ushindi wa magoli 32-10 dhidi ya Mkoa wa Mbeya.

Mchezo huo ulichezwa katika viwanja vya shule ya Sekondari wasichana Tabora,ukifuatiwa na mchezo mwingine kati ya Mikoa ya Mwanza na Lindi, ambapo Mwanza waliibuka washindi kwa magoli 30-8.

Michezo mingine iliwakutanisha Kilimanjaro na Ruvuma wasichana, na matokeo kuisha kwa Kilimnjaro kuibuka na ushindi wa 14-7, huku Dar es salaam iliibuka na ushindi wa 18-6 dhidi ya Arusha.

Mchezo mwingine wa Wasichana ulishuhudia wenyeji Tabora kwa mara nyingine wakiibuka na ushindi wa 20-5 ilioupata kutoka mkoa wa Lindi, wakati Manyara ikikubali kufungwa 25-9 na Mkoa wa Geita.

Aidha katika mchezo mwingine timu ya Mkoa wa Morogo wavulana iliifunga Mkoa wa Ruvuma magoli 29-12, michezo yote ikiwa imechezo katika viwanja vya shule ya sekiondari Tabora Wasichana.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…