BRYSON MSHANA, TABORA
Timu za wasichana kutoka mikoa mbalimbali zimeendelea kushindana kwenye mchezo wa Netiboli, katika mshindano ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea mkoani Tabora.
Katika michezo iliyochezwa leo tarehe 5 Juni 2023 majira ya asubuhi kwenye viwanja vya shule ya wasichana Tabora, Timu ya Netiboli kutoka Mkoa wa Mbeya iliibuka na ushindi magoli 26 dhidi ya Unguja iliyopata magoli 15.
Mchezo mwingine ulizikutanisha Timu za Mikoa ya Arusha na Mtwara, ambapo Arusha ilishinda magoli 28 huku mtwara ikipata magoli 13.
Wakati Arusha ikiibuka na ushindi huo, Majirani zao Mkoa wa Kilimanjaro waliwaadhibu Iringa kwa jumla ya magoli 31- 10, Tanga kuibuka na ushindi magoli 22 – 19 dhidi ya mkoa wa Singida.
Michezo mingine iliikutanisha Mikoa ya Katavi na Kagera, ambapo ilipoteza kwa magoli 28 kwa 18, na Mkoa Kigoma kukubali kipigo cha magoli 21 – 19 kutoka kwa wenzao wa Mkoa wa Rukwa.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






