BRYSON MSHANA, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.co
Wakala wa Usajili na Biashara (BRELA), wakishirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na wizara ya uwekezaji na viwanda, wamepongezwa kwa kutoa mafunzo ya maafisa  biashara 100 kutoka mikoa 10 ya Tanzania Bara yaliyofanyika Mkoani Mtwara.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Boma Mjini Mtwara Mei 12, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas  amewapongeza BRELA na maofisa biashara hao, na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kujiboresha katika utendaji wao wa kazi.
“Ninawashukuru na kuwapongeza waandaji wa mafunzo haya ya sheria za biashara na nawapongeza walioteuliwa kuja kushiriki mafunzo haya hii ni fursa kubwa na muhimu kwa maafisa kuijua sheria ili iwasaidie katika kazi.” Amesema Kanali Abbas.
Naye kaimu mkuu wa  sehemu za leseni za biashara wa Brela, Tawi Godfrey Kilumile, amesema wameandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na wizara ya uwekezaji viwanda na biashara  ambapo ni mafunzo ya sheria ya leseni za biashara na sheria ya taifa ya usajili na utoaji wa leseni za viwanda.
“mafunzo haya yanafanyika kwa maafisa biashara kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa wa sheria yenyewe lakini pia kuimarisha na kuboresha utendaji kazi wa maafisa biashara ambao ndio Wapo karibu katika kuwasimamia na kuwashauri pamoja na kuwaelekeza wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali.”
“mafunzo haya ambayo yamefanyika kanda ya kusini yamewakutanisha maafisa biashara 100 kutoka mikoa 10 ambayo ni kanda ya kusini na nyanda za juu kusini tumefanya muendelezo wa kutoa mafunzo, awali tulishafanya kwa maafisa 300 kutoka Tanzania bara lengo kuu ni kuimarisha sheria na utendaji kazi.“amesema Kilumile.
Nao baadhi ya maafisa biashara walioshiriki mafunzo hayo ya siku tatu akiwamo, Sada Salumu Lukaya kutoka halmashauri ya wilaya ya Nyasa  amesema mafunzo hayo yamemsaidia kuijua sheria ya biashara vizuri na ataenda kuwajibika vizuri hasa kwa  wafanyabiashara ambao leseni zao zimeisha muda wake na hawaendi kulipia leseni mpya.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…