MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
mtwarapressclub@gmail.com
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga, amesema lengo la TASAF ni kuhakikisha ushirikishwaji kaya za watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa unahusisha nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Aprili 13, 2023 kwenye mkutano wa Kikao kazi Cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa amesema lengola kikao hicho ni kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa.
“Serikali kupitia mpango huu imeamua kutoa ruzuku Maalumu kwa kaya za watu wenye ulemavu Ili kuwaongezea uwezo wa kufanya majukumu yao,”. Amesema Ladslaus Mwamanga.
kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzana Mayengo amsema ujumuishaji na uimarishaji kwa watu wenye ulemavu utaliwezesha kundi hilo kupata maendeleo na kuondokana na umasikini
Ameutaka mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuhakikisha inajumuisha na kuimarisha kaya za watu wenye ulemavu Ili kuwezesha kundi hilo kupata maendeleo

Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzana Mayengo akizungumza katika kikao hicho Ap[ril 13, 2023.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan Iko mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na umasikini sambamba na kushiriki Shughuli mbalimbali za maendeleo
Naye Mwenyekiti wa Shirikusho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania Ernest Kimaya ameshukuru serikali kwa kushirikisha watu wenye ulemavu kwenye mpango huu ambapo kwa sasa kundi hilo limekuwa likiweza kutoa mchango kwa familia zao
Hata hivyo ameionba serikali kuangalia namna ya kusaidia kundi la watu wenye ulemavu kwenye nafasi za ajira pindi fursa zinapopatikana
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






