ANDREA NGOBOLE, ARUSHA

mtwarapressclub@gmail.com

Harakati za kugombea ujumbe wa halmashauri kuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha zimeanza kwa Vigogo wa chama hicho kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo nyeti kwa chama tawala nchini Tanzania.

Fomu hizo zimeanza kuchukuliwa Machi 23 na wanachama wa chama hicho  ambapo mwanachama wa kwanza kujitokeza  kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) James ole Millya.

Wakili Olle Millya akionesha Fomu ya    kugombea ujumbe wa NEC CCM mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha

Olle Millya ambaye kwa sasa ni mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Africa MAshariki (EALA) anasema  ana uzoefu wa muda mrefu na siasa za mkoa wa Arusha ambazo zinahitaji vijana imara kama yeye kuwezesha kushinda majimnbo ya mkoa huo kwani amekuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na mbunge wa jimbo la Simanjiro.

Amesema yeye kama kijana aliyepikwa na chama amejitokeza kuwania nafasi hiyo ili kusaidia chama kushinda kwani anajua vema siasa za nchi ya Tanzania na asingependa kusikia jimbo la Arusha ni la upinzani bali jimbo ni mali ya Ccm kama ilivyo sasa.

Amempongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuruhusu mikutano ya Vyama vya Siasa hivyo kutokana na uzoefu wake katika nafasi zake alizokuwa nazo awali anaamini akipata nafasi ya ujumbe wa Halmshauri kuu atasaidia Chama.

“Ninauzoefu wa kisiasa na naomba ridhaa ya kuwania nafasi hii kwani sifa na uzoefu wa pande zote mbili katika chama ninao”

Milya ni Miongoni mwa vijana machachari wenye historia kubwa sana katika siasa na uongozi Mkoania Arusha na sasa anajaribu kuomba nafasi ya kugombea ujumbe wa NEC .

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…