ANDREA NGOBOLE, ARUSHA
Kampuni ya usambazaji wa mbegu ya Balton Tanzania,imezindua mbegu mpya ambazo zinaweza kukabiliana na Ukame nchi ili kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali na hivyo kuuza mazao nje ya nchi.
Akizungumza katika uzinduzi wa mbegu hizo na mafunzo ya Shamba darasa kwa wakulima tarehe 8 Machi 2023 , Mkurugenzi Mtendaji wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania(TASTA) Bob Shuma, amesema mbegu bora ndio Suluhu ya kuongeza Uzalishaji wa chakula.
Shuma amewataka wakulima kujifunza matumizi ya mbegu bora ili kuongeza uzalishaji wa mazao.yao.
Amesema, mbegu bora ambazo zinazalishwa na taasisi ya Balton Tanzania na taasisi nyingine zikitumiwa vizuri, Tanzania itakuwa na uwezo wa kuongeza uzalishaji wa chakula na hata kuuza nje na hivyo kuongeza mapato ya kigeni.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Balton Tanzania na Rwanda, Chris Keeping amesema kama wakulima nchini Tanzania, wakipata mbegu bora wanaweza kuongeza uzalishaji wa chakula na hivyo kuuza nje mazao yao.
Keeping amesema mbegu ambazo wameanza kuzisambani za za nyanya, vitunguu,pilipili hoho,., kabeji , tikiti maji na mboga mboga ili wakulima wazitumie mbegu hizo kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali na kuweza kuuza mazao nje ya nchi”alisema
Meneja wa Balton Tanzania, Ravi Periyasamy amesema taasisi hiyo, itaendelea kutoa mafunzo kwa wakulima na wasambazaji mbegu nchini,ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.
Periyasamy mbegu mpya ambazo zimeanza kusambazwa na taasisi hiyo, zinazingatia athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yamesababisha kupungua kwa uzalishaji wa chakula.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






